DAR ES SALAAM COLLEGE OF HOTEL AND BUSINESS STUDIES

DAR ES SALAAM COLLEGE OF HOTEL AND BUSINESS STUDIES
P.O BOX 40015, TANZANIA EAST AFRICA NAFASI ZA MASOMO YA HOTEL, TOURISM& BUSINESS CERTIFICATE AND DIPLOMA COURSE IN 1. Hotel Reception and front office 2. Food science and Beverage services 3. Tourism and Travel studies 4. Hotel House keeping 5. Food Production Cooking and Bakery 6. Clearing and forwarding 7. Computer studies and Maintenance 8. Accounting 9. Business Administration 10. Procurement & Supply 11. Human Resource Chuo kimesajiliwa NACTE Reg No (BMG/054P) KwaMawasilianozaidi: 0713-601763, 0755-823449, 0789-0447442, 0767-929110

Alikiba kuzindua mbili Uwanja wa Taifa


Alikiba kuzindua mbili Uwanja wa TaifaMKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Kiba ‘Alikiba’, anatarajia kulitumia Tamasha la Matumaini 2014 kuzindua rasmi nyimbo zake mbili zinazotikisa anga la Bongo Flava kwa sasa za ‘Mwana’ na ‘Kimasomaso’, huku akikiri kufarahishwa na mapokezi ya singo hizo kwa mashabiki nchini.
Tasnia ya muziki huo nchini kwa sasa imegubikwa
na gumzo la kazi hizo mbili za Alikiba, , alizofanyia katika studio mbili tofauti za Combination Sound chini ya mtayarishaji mahiri Man Walter na MJ Records chini ya Marco Chali.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Tanzania Daima, Alikiba alisema kuwa Tamasha la Matumaini lina maana kubwa kwake na kila Mtanzania, hivyo ameamua kulitumia kuzindulia nyimbo hizo, zilizomrejesha kwa kasi baada ya kimya kirefu kilichotokana na harakati tofauti.
“Tamasha la Matumaini, kama jina lake lilivyo ni maalum kurejesha matumamini kwa waliopoteza. Niliwahi kupoteza matumaini ya harakati zangu huko nyuma wakati naanza tasnia hii, lakini kupitia kitu kama hiki, nikaweza kusimama na kuwa Alikiba mwenye jina na mafanikio niliyonayo sasa,” alisema mkali huyo.
Aliongeza kuwa kwa kutambua hilo amewataka Watanzania kumiminika kwa wingi Uwanja wa Taifa Agosti 8, kushuhudia shoo kali atakayofanya sanjari na nyota wengine wa muziki huo watakaotumbuiza katika tamasha hilo, ambalo litawarejeshea matumaini katika nyanja na tasnia tofauti walizomo.
Alisema baada ya tamasha, ataanza rasmi mchakato wa kuandaa video ya vibao hivyo, alivyovitaja kuwa ni zawadi maalum kwa mashabiki wake, ambao walimpa wakati mgumu akitafakari namna ya kutii kiu.
“Kimya kingi kina mshindo mkuu kaka. Nilibanwa na masuala mbalimbali, kama vile michakato ya kibiashara, mapumziko maalum yaliyotokana na kufululiza muziki kwa muda mrefu na pia kumpaisha bwana mdogo (Abdul Kiba). Sasa niko kamili, hakuna kulala wala kupumzika tena, ni ‘non-stop’ kwa kwenda mbele,” alisema Alikiba.