Ikiwa ni siku chache zimepita baada ya mwigizaji Kajala kudai kuwa mrembo Wema Sepeteu ni Mnafiki,
hatimaye Mwanadada Wema Sepetu , amemlipua aliyekuwa shosti wake,
Kajala Masanja ‘K’ ambaye wiki iliyopita alimwita mnafiki, habari
ambayo ilisambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Katika habari hiyo, Kajala alikaririwa akisema kwamba licha ya
watu wengi kuamini wamepatana, hakuna ukweli kwani rafiki yake huyo ni
mnafiki kufuatia kutomthamini na kutokuwa karibu naye kama zamani
likiwemo suala la kumsifia mtu ambaye alikuwa na ugomvi na Kajala
(Dacutee).
Akizungumza na mwanahabari wetu, Wema
alisema alishangaa kuona
Kajala anamwita mnafiki wakati hakuwahi kupatana naye tangu
walipotofautiana kipindi cha nyuma kama alivyosema.
“Nashangaa Kajala ananiambia mimi ni mnafiki ‘ok fine’ na huo
unafiki wangu unakuja pale nilipomu-wish Dacutee siku yake ya kuzaliwa,
alitakaje eti? Yaani kwa kuwa yeye ana bifu la kumchukulia bwana’ke na
mimi nijiingize kwenye bifu lao?
“Au tofauti zangu mimi na yeye, Aunty Ezekiel aingilie, itakuwa
sahihi kweli kama wanavyofanya hao watu wake anaozurura nao siku hizi?
Wanaingilia vitu ambavyo hawavijui kiundani wake? Nasema siyo sahihi
kabisa mimi nitabaki kama Wema Sepetu na yeye atabaki kama Kajala
Masanja na asifikirie kuwa nitakuja kuwa kama zamani na yeye halafu kama
anamaindi kuhusiana na Dacutee mbona Petit Man ambaye ana uhusiano naye
aliweka picha ya Dacutee na kumu-wish hajammaindi?” aliwaka Wema.
Akiendelea kutema cheche, Wema alisema anachopaswa kuzungumza Kajala ni ukweli wa matatizo yao na siyo kusingizia watu wengine.
“Mbona siku ile niliwahadithia kila kitu (waandishi) kuhusiana
na tatizo letu, si nimetoa kinyongo changu ambacho nilikuwa nacho siku
nyingi hivi sasa najiona mwepesi na kama na yeye anataka kusafisha moyo
wake anatakiwa afunguke, kuanzia leo nataka niseme sitaki kusikia na
kuulizwa suala la mimi na Kajala kwani nimechoka na nina mambo mengi ya
kufanya,” alisema Wema.
Akizungumzia ishu ya kukutana na Kajala na kupiga picha za
pamoja wakiserebuka hivi karibuni, Wema alisema alifanya vile kuonesha
kwamba hana kinyongo na ndiyo maana alivyoombwa apige picha na Kajala,
hakusita kufanya hivyo.
“Mimi ni mtoto wa Kiislamu na nina imani na upendo kwa kila mtu,
siwezi nikamkatisha mtu furaha yake na ndivyo ilivyotokea, niliombwa
nipige picha ya pamoja na Kajala siku ile ya shughuli na nilifanya hivyo
baada ya pale nikaenda zangu kulala,” alimalizia kusema Wema.
Bifu la mastaa hao wakali wa Bongo Movies liliibuka baada ya
Wema kumtuhumu Kajala kuwa ametembea na aliyekuwa bwana’ke, kigogo
aliyetajwa kwa jina la CK
DAR ES SALAAM COLLEGE OF HOTEL AND BUSINESS STUDIES

P.O BOX 40015, TANZANIA EAST AFRICA NAFASI ZA MASOMO YA HOTEL, TOURISM& BUSINESS CERTIFICATE AND DIPLOMA COURSE IN 1. Hotel Reception and front office 2. Food science and Beverage services 3. Tourism and Travel studies 4. Hotel House keeping 5. Food Production Cooking and Bakery 6. Clearing and forwarding 7. Computer studies and Maintenance 8. Accounting 9. Business Administration 10. Procurement & Supply 11. Human Resource Chuo kimesajiliwa NACTE Reg No (BMG/054P) KwaMawasilianozaidi: 0713-601763, 0755-823449, 0789-0447442, 0767-929110