Sarah ameanza kutamba katika muziki wa Injili jijini Mwanza na sasa anakaribia kuiteka Tanzania kwa ujumla, amepiga hodi visiwani Zanzibar na anatarajia kufanya tamasha kubwa huko Zenji.
Mratibu wa maonyesho yake Paskal Linda amesema ujio wa mwanadada huyo katika injili na dhahili Rose Muhando amepata mpinzani wake, 'Kusema kweli Sarah Bagumhe anajua kutunga na kuimba hivyo ushindani wa kweli unaweza kuwepo', alisema Linda.
Msanii huyo tayari amerekodi album yake ya audio na video inayokwenda kwa jina 'Ni vizuri kumshukuru Mungu', albam hiyo inajumuhisha nyimbo nane, nyimbo zilizomo ni pamoja na Ni vizuri kumshukuru Mungu ambayo inabeba jina la albamu hiyo, ufanane na nani ?, Mwoyo gwange, nena rohoni, nipe maji, tulina omukwano, nipe nguvu na tupapoomba.
Nyimbo zote zimefanywa na kampuni ya GTC Media ya Kisumu nchini Kenya, akizungumza zaidi Sarah amesema 'kwanza namshukuru Mungu kwa kumaliza mwanzo wa kazi hii pia na wote walio nisaidia kufika mpaka hapa, pia naomba sana wapenzi wa injili wasubirie kwa hamu video ya 'Ni vizuri kumshukuru Mungu', ambayo itakuwa ni nzuri kuliko na inatarajia kuwa hewani mwezi ujao` alisema. www.palimude.blogspot.com