DAR ES SALAAM COLLEGE OF HOTEL AND BUSINESS STUDIES

DAR ES SALAAM COLLEGE OF HOTEL AND BUSINESS STUDIES
P.O BOX 40015, TANZANIA EAST AFRICA NAFASI ZA MASOMO YA HOTEL, TOURISM& BUSINESS CERTIFICATE AND DIPLOMA COURSE IN 1. Hotel Reception and front office 2. Food science and Beverage services 3. Tourism and Travel studies 4. Hotel House keeping 5. Food Production Cooking and Bakery 6. Clearing and forwarding 7. Computer studies and Maintenance 8. Accounting 9. Business Administration 10. Procurement & Supply 11. Human Resource Chuo kimesajiliwa NACTE Reg No (BMG/054P) KwaMawasilianozaidi: 0713-601763, 0755-823449, 0789-0447442, 0767-929110

Mmea wa kukuza sehemu za siri wagundulika




KWA kutumia mabango, lengo likiwa kutangaza kazi zao, waganga wengi wa tiba asilia wamekuwa wakijinadi kuwa wanatoa tiba ya kurefusha maumbile ya siri ya wanaume, kukuza makalio au matiti.
Katika mitaa ya miji na majiji nchini, siyo jambo la ajabu kukutana na mabango hayo, ambayo hata hivyo kushamiri kwake kunaleta picha kwamba ni kutokana na uhitaji mkubwa wa huduma hiyo nchini, huku watoa huduma husika wakinufaika kwa kujikusanyia kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa wahitaji.
Pia dawa zinazodaiwa kukuza makalio maarufu kama ‘mchina’, zimekuwa gumzo baada ya kuingia nchini, huku zikielezwa kukosa ubora na kwamba zina madhara makubwa.
Lakini, sasa unaweza kuachana na dawa hizo za Kichina, baada ya kugundulika mmea wenye uwezo wa kukuza makalio, matiti, pamoja na kurefusha uume.
Taarifa za kiutafiti zinautaja mti huo kwa jina la Mvunge, ukiwa na uwezo wa kukuza makalio, matiti na kurefusha uume.
Kaimu Msajili wa Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, Dk Naomi Mpemba anasema kuwa mmea huo ambao huwa ni mti mkubwa upo na kwamba una uwezo mkubwa wa kukuza maumbile hayo.
Anabainisha kuwa mmea huo ambao hukua na kuwa mti mkubwa huzaa matunda yanayotumika kama dawa na unapatikana wilayani Korogwe Mkoa wa Tanga, Pwani, Mbeya, Morogoro na baadhi ya mikoa nchini.
“Tulifuatilia na kutambua kuwa mti huo upo maeneo hayo na unatumiwa zaidi na waganga, hata picha za mti huo tunazo,” anasema Dk Mpemba na kuongeza:
“Jina jingine unaitwa Miegeya, mara nyingi unastawi katika maeneo yenye ardhi ya unyevunyevu, una tabia ya kustawi kama Mwembe na matunda yake huonekana kufanana na Mbuyu.” wiki ijayo www.afrikayaleo.blogspot.com itawaletea wataalamu wa miti shamba na simuzao ili muweze kuwatafuta wenyewe kwahuduma hizi.