DAR ES SALAAM COLLEGE OF HOTEL AND BUSINESS STUDIES

DAR ES SALAAM COLLEGE OF HOTEL AND BUSINESS STUDIES
P.O BOX 40015, TANZANIA EAST AFRICA NAFASI ZA MASOMO YA HOTEL, TOURISM& BUSINESS CERTIFICATE AND DIPLOMA COURSE IN 1. Hotel Reception and front office 2. Food science and Beverage services 3. Tourism and Travel studies 4. Hotel House keeping 5. Food Production Cooking and Bakery 6. Clearing and forwarding 7. Computer studies and Maintenance 8. Accounting 9. Business Administration 10. Procurement & Supply 11. Human Resource Chuo kimesajiliwa NACTE Reg No (BMG/054P) KwaMawasilianozaidi: 0713-601763, 0755-823449, 0789-0447442, 0767-929110

Muhando: Uzinduzi wa ‘Pindo la Yesu’ utatisha

Muhando: Uzinduzi wa ‘Pindo la Yesu’ utatisha MALKIA wa muziki wa injili nchini, Rose Muhando, amesema maandalizi ya uzinduzi wa albamu yake ya ‘Kamata Pindo la Yesu’, yanakwenda vizuri.
Akizungumza kwa njia ya simu, Muhando alisema kwa sasa yupo katika maandalizi ya mwisho kwani uzinduzi huo utakaofanyika Agosti 3, katika Ukumbi wa
Diamond Jubilee, anataka uwe tofauti.
“Katika safari yangu ya huduma ya uimbaji, nimefanya uzinduzi mara nyingi, lakini huu wa safari hii nataka uwe wa tofauti kabisa,” alisema Muhando.
Alisema kwa kutambua kiu ya wapenzi na mashabiki wake, hata waimbaji watakaomsindikiza siku hiyo, wakiwemo Anastazia Mukabwa wa Kenya, John Lisu na wengine mahiri wamekuwa katika maandalizi ya aina yake.
Muhando alisema hana hofu na uzinduzi huo ambao anaamini utakuwa wa kihistoria, hasa baada ya Kampuni ya Msama Promotions chini ya Mkurugenzi Alex Msama kutoa sapoti yake kwa njia ya udhamini.
Alisema baada ya moto wa siku hiyo katika ukumbi wa Diamondi Jubilee, makali yatageukia katika mikoa mbalimbali.