MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Kiba, amesema msanii
mwenzake wa muziki huo, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ hawezi kuziba
nafasi yake.
Kauli hiyo ya Alikiba imekuja baada ya kutakiwa kuelezea
alivyojipanga katika ujio wake mpya katika muziki huo kutokana na
kuonekana kwamba nafasi
ambayo alikuwa nayo kwa miaka ya nyuma sasa
inashikiliwa na Diamond.
“Hakuna aliyechukua nafasi yangu katika tasnia ya muziki, yani kama
ni kiti basi kina vumbi, ninachokifanya ni kukipangusa na kukikalia
tena, kila mmoja ana nafasi yake, hivyo sijaona bado aliyechukua nafasi
yangu,” alisema Alikiba.
Alisema kuwa alikuwa ameamua kupumzika tu sio kwamba anaogopa
ushindani, na kuongeza kuwa sasa yupo katika hatua za mwisho za
maandalizi ya ngoma yake mpya inayojulikana kwa jina la ‘Dar es
Salaam’ ambayo ndani yake ameelezea jinsi vijana wanavyojiingiza katika
janga la dawa za kulevya.
Alikiba alisema ameamua kutoa wimbo wa kuwahamasisha vijana wenzie
waachane na utumiaji wa dawa za kulevya kwani zinapoteza wengi na
hazina faida yoyote. Anaamini kwa kufanya hivyo kuna ambao wataepuka.
DAR ES SALAAM COLLEGE OF HOTEL AND BUSINESS STUDIES

P.O BOX 40015, TANZANIA EAST AFRICA NAFASI ZA MASOMO YA HOTEL, TOURISM& BUSINESS CERTIFICATE AND DIPLOMA COURSE IN 1. Hotel Reception and front office 2. Food science and Beverage services 3. Tourism and Travel studies 4. Hotel House keeping 5. Food Production Cooking and Bakery 6. Clearing and forwarding 7. Computer studies and Maintenance 8. Accounting 9. Business Administration 10. Procurement & Supply 11. Human Resource Chuo kimesajiliwa NACTE Reg No (BMG/054P) KwaMawasilianozaidi: 0713-601763, 0755-823449, 0789-0447442, 0767-929110