
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Dodoma, David Misime, ajali hiyo ilitokea juzi majira ya saa 9:00 usiku, ikihusisha gari namba IT 7945 aina ya Toyota Nadia likiendeshwa na Edson Mwakabungu (31), mkazi wa Tabata, Dar es Salaam na lori linalodaiwa kuwa Fuso.
Kwamba katika ajali hiyo ilitokea katika barabara ya Morogoro – Dodoma eneo la Ranchi ya NARCO, Wilaya ya Kongwa, lori hilo liliigonga kwa nyuma gari hiyo ndogo ambayo ilikwenda kugonga gema na kusasababisha watu watatu kujeruhiwa.
Aliwataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni Mwakabungu aliyelalamika maumivu sehemu za vidole vya miguu yote na Bukuku (40), mwimbaji wa nyimbo za injili, mkazi wa Tabata, Dar es Salaam anayelalamikia maumivu sehemu mbalimbali za mwili.
Majeruhi mwingine Frank Christopher (20) ambaye naye ni mwimbaji wa muziki wa injili mkazi wa Tabata, Dar es Salaam, amepata michubuko usoni na mkono wa kulia.
Kamanda alieleza kuwa majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma kwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.
Alisema walikuwa wanatokea Dar es Salaam ambapo dereva wa Fuso alikuwa anaelekea DRC.
Kamanda Misime alisema uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea ikiwa ni pamoja na kutafuta gari lililowagonga.
Akizungumzia ajali hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, Alex Msama, alisema amepokea kwa masikitiko taarifa hizo na kwa niaba ya wadau wa muziki wa injili nchini, anampa pole Bahati na wengine wote waliopata maumivu kutokana na ajali hiyo.
“Nimepokea kwa masikitiko habari za dada yangu Bukuku kupata ajali mkoani Dodoma, namtakia pona ya haraka aweze kuendelea na kazi yake ya kuitangaza injili kupitia kipaji chake cha uimbaji,” alisema Msama.