Batarokota kabila ni msukuma kutoka maeneo ya Nyamhongoro kilomita 15 kutoka jijini Mwanza. Batarokota ni mtoto wa kwanza katika familia ya Baba na Mama Beatus linda iliyopo Igoma jijini Mwanza, yenye watoto saba kwa majina ni Happy Linda ambae ni marehemu aliyefariki tarehe 9/Mai/2007 maeneo ya Mbagala jijini Dar es salaam(rest in peace sister Happy Linda),Naomi linda,Zakaria Linda (dj zhari),Yohana linda (y brain),Monical linda na Norbert Linda.
Rapper Batarokota ana mke mmojoa na watoto wanne na alifunga ndoa jumamosi ya tarehe 5/Machi/2011 katika kanisa katoriki la Mtakatifu Partic la mjini Morogoro, rapper Batarokota alifunga ndoa na Sara Abed Linda.Na kabla ya ndoa alifanikiwa kupata watoto wawili na mmoja baada ya kufunga ndoa.Watoto wanne wa Batarokota wakwanza alizaa na mchumba wake wa kwanza Saula Athony Kapama ambae kwa sasa ni marehemu aliyefariki
tarehe 9/Agosti/2005 Sumve Matare kwa ajali ya Treni ya
abiria iliyokuwa ikienda Dar essalaam, Saula Kapama alimwachia Batarokota mtoto mmoja jina Ng`wibis Linda ambae alizaliwa Agosti 2000 katika Dispensary ya St Michael iliyopo kijiji cha Igoma jijini Mwanza (rest in peace Saula Antony Kapama, mama ng`wibis ), mtoto wa pili wa Batarokota ni Shija Paskal ambae alizaliwa Desemba 2006 katika Hospital ya Bugando jijini Mwanza, Batarokota alizaa mtoto na rafiki wake wa kike Ruti Fidel Kanuti na Mtoto wa tatu wa Batarokota ni mtoto wa kike Makrina Juliana ambae alizawa Novemba/ 2011 mjini Morogoro katika Hospital ya Morogoro amezaa na na nne ni Telesia wa mtoto Yesu wa mke wake Sarah Dile Linda.
ELIMU
Batarokota amesoma shulu ya msingi Igoma, nakumaliza shule 1990 na alifanikiwa kuendelea na masomo ya sekondari 1991 katika shule ya sekondari buswelu na kufanikiwa kumaliza mwaka 1994, akiwa jijini Mwanza. Na mwaka 1995 akufanikiwa kuendelea alienda Jijini Nairobi kuendelea na chuohuko katika Chuo Cha PNG ambapo alisoma masomo wa Mziki and Design na Mwaka 1998 alimaliza. hiyo ndio muhutasalia wa elimu wa Batarokota. pia katika elimu ni mtahalamu wa kutengeneza tovuti,blogu,mashairi,hadithi,kuparfom n.k.
BATAROKOTA KWA UFUPI AMEFANYA SHOW MAENEO MENGI
Mwaka Novemba/1994 Batarokota alifanya show ya kuwaanga kidato cha nne katika shule ya Buswelu Sekondari na Mgeni rasmi alikuwa Hayati Paulo Bomani.
Mwaka, julai/1996 Batarokota alialikwa katika show ya kusaka mrembo wa Kigamboni Miss Kigamboni katika ukumbi wa CCM kivukoni .Katika show alikuwa wamealikwa wasanii Fune with Sanse kiongozi wao J- Mtambo na kundi lake la POSOJU.
Mwaka Agosti/1998 ,Batarokota alikalibishwa na kundi lake la G tha Dunia katika ukumbi wa Liberty Hall jijini Mwanza, siku hiyo walikuwa wanazingua singo ya wimbo wao 'upendo kwa mama' wasanii walio alikwa ni Mr 2, Dr KB, BWV, Makamanda wa Gola, Daz P, na wengine wengi.
Mwaka, 2004 Batarokota akiwa na kungi la G THA Dunia alialikwa pamoja na wasaniii H- Baba, J- Mo, Mr Paulo, Solo Thang, Vick Kamata na BWV. katika kufanya showkubwa iliyo fanyika katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora show hii iliandaliwa na Zizou Entertnment.
Mwaka2004 , 25,Desemba. Batarokota alialikwa yeye pamoja na msanii wa nyimbo za kiasili Mama Nyamoko (Suzana Nyamoko), kwenye show ya kuwaburudisha watu wa Geita siku ya kristimasi katika ukumbi wa Lake View Hotel .
Mwaka 2013,Machi, Batarokota amefanya show aliyo alikwa jijini Nairobi katika ukumbi wa Brokriny uliopo Gethorai 44 onyesho hili lilifadhiriwa na Princess Studio.
MAISHA YA USANII YA BATAROKOTA ..
Kipaji cha Batarokota kilianza kuonekana toka akiwa shule ya msingi Igoma mwaka 1987, Akiwa shuleni alikuwa akicheaza ngoma za asilia kwenye kundi la shule na alikuwa akifundishwa na Mwalimu Matongo ambae nimarehemu na Mwalimu Mayuyu ambae kwa sasa ni mwana kwaya wa Mtakatifu Bakita katika kanisa la Romani Katoriki Igoma.Wanafunzi ambao Batarokota anakumbuka walio kuwa wanacheza wote ngoma ni Tasi Kosinatantine, Paskal Makaka, Peter Makuke,Frimat Lyimo na wengine wengi.
Tarehe 9/Januari/1998, Batarokota alianziha kundi la mziki wa kurap jijini Mwanza kwa jina G THA Dunia, kundi hili G Tha Dunia lilikuwa ni moto wa kuotea mbali ambalo lilitikisha kanda ya Ziwa na lilikuwa likiundwa na Paskal linda a.k.a Batarokota,Juma Hassani a.k.a Big D na Danny Ngollo a.k.a Ngollo 2. Kundi hili lilifanikiwa kurekodi albamu nchini Kenya ambayo ilikuwa ikiitwa '' ONE DAY'' ambayo ilirekodiwa Agosti/1998 mjini Nairobi, Kenya katika studio ya SYNC SOUND STUDIO chini ya producer Mahamud Omari a.k.a MR MO .Album hii ya ''One Day'' ilikuwa imajazwa na nyimbo kumi ambazo ni 'one day' jina la albam,'upendo kwa mama','kiama','ogopa 666' ,'nimzuri tu','baby shake','wenyewe kwa wenyewe','watoto kwanza' ,'total balaa' na 'majonzi'. Baada ya kukaa nalo kundi hilo Batarokota aliondoka na kuachana na kundi hili 2004 na kwenda Dermank kwa ajili ya kufundisha ngoma Wadenish.
Tarehe15/,februari/2006 Batarokota alirejea kutoka Dermank na kuanzihsa kundi jipya liitwalo Watu wa Gola liliko jijini Mwanza, alianzisha kundi hili akiwa na Juma Hassani a.k.a Big D, Kundi hili Watu wa Gola walifanikiwa kurekodi nyimbo mbili 'Tumerudi' na 'vichwa vya kale' nyimbo hizi zimerekodiwa katika studio ya M.O. Record iliyopo Pasiasi jijini Mwanza chini ya mtayarishaji Q The DON na Dj Zari.
TUZO ALIZOWAHIKUPATA KATIKA SANAA
Mwaka 2001 tarehe 4/Machi msanii Batarokota akiwa na kundi lake la G THA Dunia,Kundi hili lilifanikiwa kupata zawadi ya cheti cha ushindi wa best single rap katika wimbo wa -upendo kwa mama- cheti hicho kilitolewa na Gloryhood Music Award ya jijini Mwanza .
Mwaka 2004,Octoba 22-23, Batarokota alifanikiwakupta cheti cha kuudhulia na kushiriki Music Crossroads Tanzania Workshops jijini Mwanza.
Mwaka 2014 Batarokota aliingia kwenye Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Award 2014 katika kategori ya Wimbo bora mwenye vionjo vya Asili ya Kitanzania na wimbo wake mpya wa `Kwejaga Nyangisha` fainali zilifanyika jijini Dar es salaam katika Ukumbi wa Mlimani City siku ya tarehe 3/5/2014 na Batarokota akifanikiwa kupata tuzo.
NYIMBO MPYA AKIWA NJE YA KUNDI
Msanii Batarokota kwa sasa ana nyimbo saba ambazo amesha kamilliza kwa ajili ya maandalizi ya albamu yake mpya atakayo zindua Maurtania mwezi wa sita nyimbo ambazo ziko tiyari ni ` hongera mama` and `amani` nyimbo hizi zimerekodiwa Mwaka 2003 januari katika studio Mushroom Studio jijini Nairobi Kenya chini ya mtayarishaji Teddy Karanda Harrison na Dj Zari.nyimbo vingine ni `Sukurubu` ambayo imerekodiwa Multimedia Studio jijini Mwanza mtayarishaji Kamgisha na Alon Mikomangwa wasanii walioshiriki kwenye nyimbo hii ni Ceni na Castro kutoka DRC, Kongo na nyimbo nyingineni `sauti ya haki` na `kwejaga Nyangisha` zimerekodiwa Januari,2012 studio ya Sky Studio iliyopo Kihonda Morogoro watayarishaji Orecy Owden na Julius Chares.Nyimbo nyingine ni ya kisukuma ihitwayo `irombo rise`iliyo rekodiwa 6/Decemba/2012 katika studio za Sunlight Records Mazimbu road -Kihonda Morogoro mtayarishaji King Maroh. nyimbo mpya wa mwaka huu `tanzania 2015` uliorekodiwa tarehe 12/januari/2013 katika studio ya ALNA studio iliopo nchini Maurtania chini ya mtayarishaji Alex Kalma kutoka Holand kwa udhamini wa Ilona Maurer kutoka Marekani.