Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Sarah Bagumhe alisema `kwanza namshukuru Mungu kwa kumaliza mwanzo wa kazi hii pia na wote walio nisaidia kufika mpaka hapa,pia naomba sana wapenzi wa injili wasubirie kwa hamu video ya Ni vizuri kumshukuru Mungu, ambayo itakuwa ni nzuri kuliko na inatarajia kuwa hewani mwezi ujao` alisema.
Msanii Sarah Bagumhe anaishi kwa sasa jijini Mwanza, hii ni albamu yake ya kwanza ambayo anatarajia itoke hivi karibuni katika uzinduzi utakao fanywa jijini Mwanza.