NYOTA
wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ambwene Yesaya ‘AY’ ni miongoni mwa
wasanii wa Afrika walioalikwa na Rais Barrack Obama wa Marekani
kutembelea Ikuluya nchi hiyo (White House) kwa mkutano.
Obama amewakaribisha wasanii hao kutoka Afrika katika mkutano mkubwa na viongozi mbalimbali wakuu wa nchi za Afrika, ulioanza jana na kudumu kwa siku tatu.
Kwa mujibu wa AY kupitia ukurasa wake wa facebook, wasanii wengine ambao wapo katika ziara hiyo ni Femi Kuti na D’Banji wa Nigeria, Fally Ipupa wa Congo DRC, Victoria Kimani wa Kenya na mchezaji wa Manchester City ya England, Yaya Toure ambaye ni raia wa Ivory Coast