
Akizungumza Tanzania Daima jijini Dar es salaam jana, Darasa alisema, tangu anaanza muziki amekuwa akipata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki na wadau wake ndani na nje ya nchi, hivyo ni kitu cha kujivunia kwake.
Darasa ambaye yuko katika kundi la Classic Music Group (CMG), ambalo lipo chini ya studio ya AM Records, kwa sasa anatamba na kibao chake cha
‘Sio Mbaya’, licha ya kupaya umaarufu kupitia vibao vingine kama, Sikati Tamaa, Nishike Mkono, Ukipenda Hauoni na nyinginezo.
Alisema, pia anashukuru kupata sapoti kutoka kwa mkongwe wa muziki huo nchini, Joseph Haule ‘Proffesor Jay’, kitu ambacho anajivunia.
“Nashukuru kupewa sapoti kutoka kwa nguli huyu, aliposikia wimbo wangu wa ‘Sikati Tamaa’ alinitafuta na kuzungumzia uwezo wangu katika vyombo mbalimbali vya habari, kiukweli ni kitu ambacho najivunia sana,” alisema