DAR ES SALAAM COLLEGE OF HOTEL AND BUSINESS STUDIES

DAR ES SALAAM COLLEGE OF HOTEL AND BUSINESS STUDIES
P.O BOX 40015, TANZANIA EAST AFRICA NAFASI ZA MASOMO YA HOTEL, TOURISM& BUSINESS CERTIFICATE AND DIPLOMA COURSE IN 1. Hotel Reception and front office 2. Food science and Beverage services 3. Tourism and Travel studies 4. Hotel House keeping 5. Food Production Cooking and Bakery 6. Clearing and forwarding 7. Computer studies and Maintenance 8. Accounting 9. Business Administration 10. Procurement & Supply 11. Human Resource Chuo kimesajiliwa NACTE Reg No (BMG/054P) KwaMawasilianozaidi: 0713-601763, 0755-823449, 0789-0447442, 0767-929110

Suge Knight apigwa risasi sita!




Party ya utangulizi wa utoaji tuzo za video za MTV (Pre-VMA Party) iliingia dosari baada ya CEO wa zamani wa Death Row Records alikuwa mmoja kati ya watu watatu waliojeruhiwa vibaya kwa risasi.
Kwa mujibu wa TMZ, machafuko hayo yalitokea nje ya club ya usiku ya 10AK magharibi mwa Hollywood majira ya saa saba na nusu usiku.
Suge Knight anaripotiwa kupigwa risasi sita zilizompata tumboni, mkononi na sehemu nyingine za mwili. Alikimbizwa hospitali ambapo hali yake inaripotiwa kutia matumaini baada ya kufanyiwa upasuaji.
Polisi walifika katika club hiyo na watu wote walitoka wakiwa wameweka mikono juu kufuatia tukio hilo la hatari.
Chris Brown alikuwa mshereheshaji katika party hiyo ambayo ilihudhuriwa na watu maarufu akiwemo Tyson Beckford.
Mashuhuda wameeleza kuwa kabla ya tukio hilo, rapper The Game na rafiki zake waligombana na mlinzi wa club hiyo na kukataliwa kuingia ndani. Game aliondoka na kuwaacha rafiki zake maeneo hayo.
Kufuatia tukio hilo,  Polisi wanafanya uchunguzi dhidi ya makundi mawili ya kihalifu ambayo yalikuwa na beef ya muda mrefu. Game na Suge Knight wote wanahusishwa na kundi maarufu la bloods