MKALI wa muziki wa kizazi kipya Batarokota , amesema kuwa, msanii ambaye anamkubali hapa nchini ni Nan Kize Batarokota nyota aliyerejea katika ‘game’ huku akiachia nyimbo mbili kwa mpigo, alikonga nyoyo za mashabiki wa muziki mjini Lushoto, katika tamasha la KWEKANGA siku chache zilizopita huku msanii wa bongo fleva akiwemo Nan Kize wakimsapoti alipokuwa jukwaani katika ukumbi wa Kakune.
Batarokota alibainisha hayo, alipokuwa akifanya mahojiano na www.afrikayaleo.blogspot.com siku ya jumatatu, alisema, hapa nchini kuna wasanii wengi lakini, anakunwa na uimbaji na utunzi wa Nan Kize.
Aliongeza kuwa, hapendezwi na watu ambao wanamlinganisha yeye na Mzee Mwinamira kwa kuwa ni vitu viwili tofauti, kwani uimbaji wake mzee huyo ni tofauti na wa kwake hivyo hapendi kulinganishwa naye.