DAR ES SALAAM COLLEGE OF HOTEL AND BUSINESS STUDIES

DAR ES SALAAM COLLEGE OF HOTEL AND BUSINESS STUDIES
P.O BOX 40015, TANZANIA EAST AFRICA NAFASI ZA MASOMO YA HOTEL, TOURISM& BUSINESS CERTIFICATE AND DIPLOMA COURSE IN 1. Hotel Reception and front office 2. Food science and Beverage services 3. Tourism and Travel studies 4. Hotel House keeping 5. Food Production Cooking and Bakery 6. Clearing and forwarding 7. Computer studies and Maintenance 8. Accounting 9. Business Administration 10. Procurement & Supply 11. Human Resource Chuo kimesajiliwa NACTE Reg No (BMG/054P) KwaMawasilianozaidi: 0713-601763, 0755-823449, 0789-0447442, 0767-929110

UK kuanzisha benki ya mbegu za kiume


inaelezwa kuwa benki ya mbegu za kiume itatatua haja za uzazi
Benki ya Taifa ya mbegu za kiume inatarajiwa
kuanzishwa nchini Uingereza kuondokana na tatizo la upungufu wa mbegu hizo.
Wapenzi wa jinsia ya kiume na kike , wale wa jinsia moja pia wanawake wasio na wenza watanufaika na huduma hii mpya ambapo kutoka jamii zisizofahamika watakuwa na uwezo wa kuchagua wachangiaji kutoka katika jamii nyingine
Benki hii itakayosimamiwa na Mfuko wa Taifa wa Gamete na Hospitali ya Wanawake ya Birmingham itafunguliwa mwezi Oktoba.
Mradi huu umetengewa paundi 77,000 na Idara ya Afya nchini Uingereza.
Kituo hiki kitakuwa katika hospitali ya wanawake mjini Birmingham ambacho kitakuwa kikihifadhi mbegu hizo.
Hivi sasa kumekuwa na upungufu wa wachangiaji wa mbegu za kiume nchini Uingereza hasa katika hospitali za taifa,huku kukiwa na ongezeko la uhitaji, hospitali hizo zikitibu tatizo hilo linaloelezwa kuwa kubwa nchini humo.
Mfuko huo umesema una matumaini kuwa uwepo wa benki hiyo utapunguza idadi ya wagonjwa wanaojiweka katika hatari kwa kutafuta huduma hii bila kufuata taratibu