Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Batarokota alisema amelazimika kufanya hivyo akitambua kiu ya wadau, wapenzi na mashabiki wake kutaka kuona vitu vya tofauti siku hiyo katika Ukumbi Brookrine uliopo Gethorai 44 , Nairobi nchini Kenya.
Alisema kwa mazoezi anayofanya, anaamini moto ambao atauwasha siku hiyo, utakuwa kama salamu kwa wapenzi na mashabiki wake.Msanii Batarokota ambae mwaka huu wimbo wake wa kwejanga Nyangisha uliingia katika tuzo za Kilimanjari Tanzania Music Awards 2014 katika kategori ya `Wimbo bora wenye vionji vya asili ya kitanzania` na akuweka kufanikiwa kupata Tuzo. Msanii Batarokota hii ni ziara yake ya pili mwaka 2014 kufanya show Nairobi nchini Kenya. pia waweza kupata nyimbo wa msanii Batarokota kupitia tovuti ya Mkito.com https://mkito.com/song/kwajaga-nyangisha/550