DAR ES SALAAM COLLEGE OF HOTEL AND BUSINESS STUDIES

DAR ES SALAAM COLLEGE OF HOTEL AND BUSINESS STUDIES
P.O BOX 40015, TANZANIA EAST AFRICA NAFASI ZA MASOMO YA HOTEL, TOURISM& BUSINESS CERTIFICATE AND DIPLOMA COURSE IN 1. Hotel Reception and front office 2. Food science and Beverage services 3. Tourism and Travel studies 4. Hotel House keeping 5. Food Production Cooking and Bakery 6. Clearing and forwarding 7. Computer studies and Maintenance 8. Accounting 9. Business Administration 10. Procurement & Supply 11. Human Resource Chuo kimesajiliwa NACTE Reg No (BMG/054P) KwaMawasilianozaidi: 0713-601763, 0755-823449, 0789-0447442, 0767-929110

Vick Kamata ajisalimisha kwa Yesu


Mbunge wa Viti Maalum (UVCCM) Mkoa wa Geita, Vicky Kamata akiwa na aliyekuwa mchumba wake Charles Gadner.
Kwa mara ya kwanza Mbunge wa Viti Maalum (UVCCM) Mkoa wa Geita, Vicky Kamata, amekiri kupata pigo mbele ya wachungaji kufuatia ndoa aliyotarajia kufunga Mei 24, mwaka huu kuvunjia.

Kamata alitarajia kufunga ndoa na Charles
Gadner lakini ndoa ya msanii huyo wa muziki wa kizazi kipya haikuweza kufungwa kama ilivyopangwa awali kutokana na sababu mbalimbali zilizojitokeza siku chache kabla ya harusi hiyo.

Mbunge huyo 'amefunguka' kuwa tukio hilo limemfanya kutambua marafiki wa kweli na maadui zake na kuwa hiyo ni sehemu ya mapito kwa mtu yeyote akiwa hapa duniani bila kujali umaarufu wake kisiasa na huo ni mpango wa Mungu na si wa binadamu.

Huku akibubujikwa na machozi mara baada ya kuombewa na waumini wa makanisa  ya Kiloloke katika Kanisa la Evangelical Asembliies of God (EAGT), katika ibada iliyofanyika katika kanisa lililopo mtaa wa mwembeni Kata ya Kalangalala mjjini Geita jana, alisema majaribu ni ya kila mtu.

Katika maombi hayo yaliongozwa na Mchungaji Obedi Chilala, Kamata alidai kuwa machozi hayo yametokana na uzito wa maombi yaliyotolewa kwake  kumuingia.

''Tukio hilo limenipa fursa ya kujifunza kuwatambua marafiki wa kweli na maaduzi zangu...na wapo waliojipiga vifua wakidai wao ndio wameingilia kuvuruga mpango huo nasema huo ni mpango wa mungu pekee hakuna cha mchawi au adui wala mwanasiasa  anayeweza kutekeleza hilo,''alidai Kamata huku akibubujikwa na mchozi.

Hii ni mara ya kwanza kwa mbunge huyo Kijana na machahari kuzungumzia kilichomfika tangu alipokumbwa ma mkasa huo uliosababisha kujikuta akiwa hospitalini amelazwa kwa muda na mengi kuzungumzwa juu yake ambapo katika kutoa shukrani zake alidai kuwa ni nguvu ya Mungu ndiyo iliyomlinda kupata ujasiri alionao vinginevyo isingewezekana.

''Kwa wiki mbili mfululizo magazeti yalikuwa yanaripoti juu yangu...hata hivyo tukio hilo silichukulii kama kashfa kama wengine wanavyoweza kuamini na badala yake ni sehemu ambayo kila mwanadamu hata awe maskini au tajiri au maarufu kama mimi yanaweza kumfika, hiyo ni sehemu ya mapito ya maisha na Mungu ndiye anayepanga,'' alidai Kamata.

Kadhalika alitumia fursa hiyo kama mgeni rasmi kuwashukuru wote waliomfariji wakati akiwa wodini na hata alipotoka baada ya kupewa mwaliko rasmi kufungua semina ya mafunzo ya makanisa ya kilokole katika mwendelezo wa mafunzo kuhusu ''Jenga Madhabahu ya Mungu Tanzania'' na kuiombea amani nchini

Awali akitoa mahubiri juu ya Mbunge huyo, Mchungaji Chilala kutoka Kanisa la EAGT Luabda la Shinyanga, alidai kuwa Mbunge huyo ana ujasiri wa Mungu na wa kuigwa hivyo anastahili kuongoza, kuheshimiwa na kwamba hawampigi debe kisiasa bali anastahili kwa ujasiri wake.

Aidha, kanisa limeahidi kumuunga mkono katika safari yake ndefu ya mbio za siasa huku likimuombea dhidi ya maadui zake kushindwa kwa madai kuwa kila anayefanikiwa lazima wapo maadui na kuwa yeye ni miongoni mwa wanasiasa  vijana lakini pia walio na maadui.

Katika maandalizi ya harusi hiyo yalidaiwa kuwa ni ya kifahari na yalitajwa kufikia Sh. milioni 96.
CHANZO: NIPASHE